- Nabii Shepherd Bushiri ambaye anasemekana kuwa mmoja wa wachungaji tajiti zaidi barani Afrika ameonyesha uwezo wake wa kifedha kwa kumnunulia mkewe gari aina ya Mercedes G-wagon

Ni wazi kwamba mchungaji mbishi na mwanzilishi wa Enlightened Christian Gathering Church (ECG), Malawi, Nabii Bushiri, anaweza kumudu maisha ya kifahari.

Mhubiri huyo kwa mara nyingine ameonyesha uwezo wake mkubwa wa kifedha kwa kumnunulia mkewe gari aina ya Mercedes G-wagon inayokadiriwa kugharimu Ksh12.7 million, kusherehekea siku ya kuzaliwa mwaka huu.

Habari Nyingine: Kweli huyu ni mwanamume, tazama alichowafanyia mabinti hawa

Katika video aliyoweka katika akaunti yake ya Facebook, anaonekana akitembea na mkewe kwenda katika chumba cha maonyesho ya magari, na kumwonyesha gari hilo.

Watu wengine wanaungana naye kwa kumwimbia wimbo wa kumtakia kila lema siku ya kuzaliwa kwake.

Katika picha hiyo, Nabii Bushiri anasema: "Ninakushukuru sana kwa upendo na msaada wako. Uliniamini wakati sikuwa na chochote, wakati huu ni wako kuburudika siku ya kuzaliwa kwako.

Habari Nyingine: Picha ambazo hujawahi kuona za watoto wake Gavana Hassan Joho

"Kwa niaba ya ECG, Shepherd Bushiri Investments RSA, Dubai, USA na UK, ninakutakia siku njema ya kuzaliwa.”

Subscribe to watch new videos

Subscribe to Tuko youtube channel to watch more interesting videos

Read ENGLISH VERSION

Una maoni?Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdian12gZhmpJygpaO0orbIZqSamaKqs7Z5wKaqoayllnqut8SwnGajp5Z6rMHMp6ynrZyerm6zwKugZqSRYriqssChmKuhXaW2pLTAZ5%2BtpZw%3D