-Mbunge mmoja wa Uganda amepigwa faini kwa kukojoa hadharani

-Picha za tukio hilo zilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii

-Mamlaka ya baraza la jiji la Kampala ilimfikisha mahakamani

Mahakama moja nchini Uganda imempiga faini mbunge mmoja kwa kitendo cha kukera umma cha kukojoa hadharani.

Picha zilionyesha Abraham Abiriga, mbunge wa manispaa ya Arua, akifanya kitendo hicho Jumatatu, Septemba 25. Picha hizo zilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii.

Alipigwa picha akikojoa kando ya ua la ofisi za waziri wa fedha jijini Kamplala.

Bwana Abiriga alikiri kufanya kosa hilo.

Mamlaka ya jiji kuu la Kampala lilimshtaki Abiriga chini ya sheria za jiji na amri za serikali.

Koti moja jijini Kampala imempiga faini Ush 40,000(Ksh 1,100) ambazo aliripotiwa kulipa. Kukosa kulipa faini hii kungesababisha kufungwa kwake kwa miezi miwili.

Habari Nyingine: Mama Baha kutoka Machachari amwandikia barua Uhuru Kenyatta

Katika mahojiano hapo awali, Abiriga alitetea kitendo chake akisema, “Ninawezaje kuendelea kuweka mkojo ndani yangu?”

Habari Nyingine: Margaret Kenyatta aonja maisha halisi ya umasikini kwenye kitendo hiki cha huruma

Kitendo chake kimekashifiwa sana sawia na kukejeliwa.

Read ENGLISH VERSION

Abiriga akiri kuojoa kando ya barabara – Kwenye TUKO TV

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiaoJ4fI9mq5qamZZ6rq7AsphmpZKqu6ixjJqnop%2BnlnqnrcinoGajp5Z6rLXTnqWdp12YtaJ5yq6inqqRYsKuucBmmqGZXaDCrLvJqJhmoJGZtW%2B006aj