-Mshukiwa huyo alimuuwa mamake na babake kutokana na mzozo wa kinyumbani
-Alimuuwa jirani aliyefika nyumbani kwao kumwokoa babake wakati wa mzozo huo
-Wanakijiji wenye hasira walimtandika mshukiwa huyo hadi kufa baada yake kutekeleza mauaji hayo
Polisi mjini Bungoma wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha mzozo uliosababisha vifo vya watu wanne katika wadi ya Musikoma, eneo bunge la Kanduyi.
Jamaa mmoja kwa jina Yusuf Shiundu aliwashambulia na kuwauwa wazazi wake na jirani yao Jumanne, Mei 15 baada ya kuwa na mzozo wa kinyumbani
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Habari Nyingine: Jamaa atwangwa kama burukenge kwa kung'ang'ania nyama mazishishini
OCPD wa Bungoma Kusini Aloise Orioki alisema kuwa mshukiwa huyo aliuwawa baadaye na wanakijiji wenye ghadhabu waliomtandika hadi kufa walipopata habari kuwa aliwauwa mamake na jirani aliyejaribu kuwatenganisha wakati wa mzozo huo.
Habari Nyingine: Kutana na kijana aliyemaliza chuo kikuu bila ‘kugusa’ msichana hata mmoja
“Babake aliyekimbizwa katika hospitali ya Bungoma Magharibi karibu na soko la Kanduyi alifariki akipokea matibabu.” Orioki alisema.
Mwakilishi wa wadi ya Musikoma George Makari aliitembelea familia iliyopatwa na msiba wa ghafla na kuwataka wakazi eneo hilo kutatua mizozo ya kifamilia kwa njia mwafaka badala ya kutekeleza mauwaji.
Habari Nyingine: Kioja: Mfanyibiashara apeleka panya 5 kituo cha polisi kwa kula pesa zake
“Kwangu, ni siku yenye huzuni. Nimepoteza kura nne. Tunastahili kutatua maswala ya kifamilia kwa njia tofauti. Mauaji haya yameturudisha nyuma.” Makari alisema.
Habari Nyingine: Warembo wapigana wakimgombea baba yake Diamond Platnumz
Miili ya marehemu wote ilipelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya rufaa ya Bungoma ambapo itafanyiwa uchunguzi.
Taarifa ya Titus Oteba – Ripota, kaunti ya Bungoma
Read ENGLISH VERSION
Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News
Walivyokamatwa kwa kuwa walevi na kuendesha gari | TUKO TV
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibIB6gpJmpLCZnpa6trnEZpmuppekuqJ5wLCYrq%2BRYsSixsCzoGavkaCybrrAZqGiqpGjtm63wJujmmWplnqswdSwmLCZXp3Brrg%3D