Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki nguli Hopekid, Yvonne Orio amemtambulisha mitandaoni mpenzi wake wa sasa na bila shaka wapenzi hao wanafurahia maisha yao kulingana na picha alizozichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram

Haya yanajiri takriban mwezi mmoja tu baada ya Hopekid na mwenzake DK Kwenye Beat kukashifiwa na mwanadada mmoja kutoka Nakuru kwa kushiri ngono naye na kumuambukiza ugonjwa wa zinaa kimakusudi.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Habari Nyingine: Raia 6 wa Canada kutoka familia moja waliangamia kwenye ajali ya ndege Ethiopia

Habari Nyingine: Jamaa aliyedai Roho Mtakatifu alimtabiria kuhusu kifo cha Uhuru kupimwa akili

Hata hivyo, Hopekid na Yvonne walikuwa tayari washaachana kabla ya sakata hiyo kuibuka.

Yvonne alijinyakulia mpenzi mwingine ila hakuwa akiyaweka maisha yake hadharani kwenye mitandao ya kijamii hadi alipojaliwa mtoto na jamaa huyo.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Yvonne alimshukuru Mungu kwa umbali alikotoka na kwa kumbariki na familia ya kupendeza.

" Leo nimefungua zawadi yangu, zawadi maridadi kutoka kwa Mola. Nawatakieni likizo njema familia yangu," Yvonne aliandika Instagram.

Hopekid naye alijinyakulia mpenzi mwingine ambaye alimtambulisha mitandaoni na hata kumposa.

Habari Nyingine: Uhuru amtunuku Joseph Boinnet cheo kipya, ampendekeza Hillary Mutyambai kuwa Inspekta Mkuu wa Polisi

Haijabainika iwapo wawili hao wako pamoja tangu sakata ya Hopekid kushiriki ngono na mwanadada huyo kutoka Nakuru kuibuka.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa inayoweza kubadilisha maisha ya mtu na ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690 na Telegram: Tuko news.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO TV

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjZX16gpRmmKWhqZq4tsPAZqSpnZ6vtm7DwGakrJmenrZutM6pnKShlGKursDAppmupJmotaJ5zKmcp7KZYrqxxcBmpKKskaOxorvNomWhrJ2h