- Msemaji wa serikali Cyrus Oguna amethibitisha Volker Bassen amejiunga na kikosi cha jeshi la wanamaji kwenye oparesheni ya kuopoa miili baharini
- Bassen alisema kwamba atahitaji saa mbili tu kuiondoa miili ya Mariam na Amanda habarini
- Jamaa huyo kutoka Uswidi ni mtaalam wa masuala ya kupiga mbizi
Oparesheni ya kuiopoa miili ya waathiriwa wa mkasa wa Bahari Hindi umechukua mkondo mpya baada ya mpiga mbizi tajika kutoka Uswidi kujiunga na kikosi cha Jeshi la Wana Maji.
Volker Bassen ambaye ni mshauri wa masuala ya kupiga mbizi alitangaza Alhamisi, Oktoba 3 kuwa, anahitaji saa mbili tu kuiopoa miili ya Mariam Kigenda na mwanawe Amanda.
Habari Nyingine: Raila asema pesa zimemwagwa Kibra kuharibu uchaguzi
Msemaji wa serikali Cyrus Oguna alithibitisha haya katika mazungumzo na NTV Ijumaa, Oktoba 4 na kusema kuwa Bassen atashirikiana na jeshi hilo kwenye oparesheni hiyo.
"Tayari kunao wapiga mbizi baharini ambao wanapiga darubini maeneo ambayo tunahisi huenda miili hiyo ikawa. Ndio, tutashirikiana na mpiga mbizi huyo wa binafsi (Volkar Bassen) na tunamkaribisha. Atachapa kazi akitumia vifaa maalum akiongozwa na Jeshi la wana maji," Ogun alisema.
Mariam na mwanawe walikumbana na mauti baada ya gari lao kudondoka kutoka kwa feri na kutumbukia baharini katika kivukio cha feri Likoni Jumapili, Septemba 29.
Habari Nyingine: KURA yatangaza kufungwa kwa sehemu ya barabara ya Outer Ring Jumapili
Mtaalam huyo ambaye ni mmiliki wa kampuni ya East Africa Whale Trust iliyoko eneo la Diani ni mkaazi wa humu nchini na amemuoa binti ya mwanasiasa.
Bassen alifichua kuwa ana vifaa maalum ambavyo atavitumia katika kubaini ni sehemu ipi haswa ambapo miili hiyo ipo kando na gari la waathiriwa.
Kupitia mitandaoni, Shirika la Feri limekuwa likitoa wito kwa Wakenya kuwa watulivu huku zoezi hilo likiendelea.
Wataalam walisema kuwa eneo lililoko gari hilo ni takriban mita 60 baharini humo ila shughuli nzima imetatizika kutokana na hali mbaya ya hewa.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjZoR0g5RmpKSZo5Z6uK2MpaCkp56eeq68yKCYZqWSnseqedaaZK6rp56xqnnAo6CuppeWeqyt06KimmWfpa6zsdKhnKehXa6ubrfUqKeomV2itqq4yGawmmWnlq61tMiroLCZXp3Brrg%3D