- Kuria anasema serikali ya Jubilee ilianza kupuuza amri ya mahakama baada ya Raila kuanza kufanya kazi pamoja na Uhuru

-Anadai kwamba Raila anatumia uchawi kumfanya Rais kutotii amri

- Mbunge huyo alikamatwa mnamo Ijumaa lakini aliwachiliwa huru siku iliyofuata licha ya mahakma kumkabithi dhamana siku ya Ijumaa

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria amedai kwamba ukaidi wa serikali umechangiwa na kiongozi wa ODM Raila Odinga.

Akizungumza mnamo Jumapili, Januari 12, katika Kaunti ya Uasin Gishu, Kuria alisema katika miaka ya awali, serikali imekuwa ikifuata amri ya mahakama lakini hayo yalibadilika baada ya maafikiano kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Raila.

Habari Nyingine: DP William Ruto afungiwa nje ya makazi yake ya kifahari Mombasa

Habari Nyingine: Aston Villa vs Man City: Aguero aandikisha historia huku City wakiponda Villa

Mbunge huyo alizua kuwa Raila alimroga Uhuru na matokeo yake yamekuwa kukaidi maelekezo ya korti.

"Raila ameroga Uhuru. Amemshauri amuhangaishe Naibu Rais William Ruto ili kupenya kwa urahisi kupata madaraka. Uhuru alikuwa mwanamume ambaye alikuwa anatambuliwa kwa kuheshimu mahakama,

"Hakuwa na shida yoyote wakati matokeo yake ya uchaguzi yalitupiliwa mbali 2017 na uchaguzi huo kurudiwa. Pia alikuwa anaheshimu vikao vya vya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) wakati alikuwa na kesi huko," alisema Kuria.

Habari Nyingine: Wakenya wamfokea Rais Uhuru, wateta hali ya kiuchumi

Kuria alitoa matamshi hayo baada ya kuachiliwa huru kutoka kwa seli ya polisi kufuatia kukamatwa kwake siku ya Ijumaa, Januari 10, kwa madai ya kumpiga mwanamke mmoja wakati wa mahojiano ya runinga.

Siku hiyo ya kukamatwa kwake, mahakama ilimkabithi dhamana ya KSh 50,000 lakini aliwachiliwa siku iliyofuata mnamo Jumamosi, Januari 11.

Kulingana na Kuria, afisa anayesimamia Kituo cha Polisi cha Kilimani alikataa kumruhusu kuondoka kama mahakama iliyokuwa imeagiza kwa kudai kwamba alikuwa anasubiri amri kutoka kwa Rais.

"Mahakama iliniwachilia kwa dhamana, lakini nilishangazwa na OCS kukataa kuniwachilia. Alisema alikuwa anangoja mawasiliano kutoka Jumba la Harambee," alisema Kuria.

Mbunge huyo pia aliguzia masaibu ya wakili aliyefurushwa nchini Miguna Miguna ambaye bado hajarejea nyumbani licha ya amri tatu iliyotolewa na korti kwa serikali kufanikisha kurejea kwake.

"Miguna sio rafiki yangu kisiasa lakini amri ya kufanikisha kurejea kwake inatakiwa kuheshimiwa. Sheria yatakiwa kukumbatiwa na hata maadui wako," alisema Kuria.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjaIF0hJZmpJutnpyybrnOrJysZZuqv6qtjJqkpJmjnbanwYyrmKKkkWK4uK2MpKymqp%2Bcrm6%2BwKKqZq2Yqr%2B2esetpKU%3D