Magazeti ya Jumanne, Julai 21, yanaripotia kuongezeka maradufu kwa maambukizi ya virusi vya corona nchini huku Wizara ya Afya ikionya kuwa seckta hiyo itafurika. Rais Uhuru Kenyatta ameitisha mkutano na magavana kutathmini mikakati ya usalama iliyolegezwa.
Kamati mpya ya Bunge la Kitaifa imeahidi kushinikiza kutekelezwakwa kwa mabadiliko katika sheria za uchaguzi na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).
Habari Nyingine: Rais Magufuli asema Tanzania imekandamiza COVID-19 na sasa watalii wanamiminika
Habari Nyingine: Mwanahabari wa Kenya,Samuel Okemwa akamatwa kwenye mpaka wa Tanzania
The Star
Bunge la Kitaifa limewekwa katika marufuku ya kutoingia na kutoka baada ya wafanyakazi 50 kupatwa na virusi vya corona.
Afisi za wabunge hao zilifungwa na wafanyakazi wote kuagizwa kufanyia kazi zao nyumbani ili kuzuia maambukizi.
Spika Justin Muturi alipiga marufuku vikao vyote vya kamati za Bunge hadi Julai 28, wakati taarifa rasmi kuhusu kudhibitiwa kwa virusi hivyo itatolewa.
Hali tete pia inashuhudiwa katika Gereza la Viwandani baada ya ripoti kudokea kwamba wafungwa 84 walipatwa na virusi hivyo.
Idadi jumla ya maambukizi nchini imefikia 13, 771 huku ya maafa ikifika 238.
The Standard
Viongozi wa kisiasa wamekuwa wakaidi katika kukiuka sheria za kudhibiti virusi vya corona iliyowekwa na Wizara ya Afya ili kukabili ueneaji.
Shughuli za kisiasa hususan katika maeneo ya Magharibi mwa Kenya ni dhahiri sheria zimekiukwa huku serikali ikishindwa kuwajibika pakubwa katika kukabili hali hiyo.
Mnamo Jumatatu, Julai 20, mawaziri Eugene Wamalwa (Ugatuzi), James Macharia (Uchukuzi), Peter Munya (Kilimo), magavana Wycliffe Oparanya (Kakamega), Wycliffe Wangamati (Bungoma) waliandaa mkutano eneo la Nzoia kujadili masuala ya sukari na maendeleo.
Seneta wa Nairobi, Johnson Sakaja ambaye alikuwa anaongoza kamati ya Seneti kuhusu janga la virusi vya corona alilazimika kujiuzulu baada ya kukamatwa akibugia pombe katika baa moja saa za kafyu.
Daily Nation
Wenyekiti wa kamati mpya ya Bunge la Kitaifa wameahidi kushinikiza mabadiliko makubwa ili kuhakikisha kuwa Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa Upinzani Raila Odinga wanaafikia malengo yao.
Mwenyekiti wa Kamati kuhusu Haki, Muturi Kigano na naibu wake Otiende Amollo wameapa kubadilisha sheria za uchaguzi na Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi.
Otiende alisema kuwa njia pekee ya kuhakikishiwa kutakuwa na kura ya wazi na amani mwaka 2022 ni kwa kusafisha tume hiyo pamoja na sheria za uchaguzi.
People Daily
Sehemu ya madiwani wa Kirinyaga walilazimika kukimbilia usalama wao baada ya vijana wenye hamaki kuwafumania na kusambaratisha mkutano wao eneo la Mwea.
Mawakilishi hao wa wadi ambao ni wanachama wa kamati kuhusu kilimo katika kaunti hiyo walikuwa wamezuru eneo hilo katika misheni ya kupata ukweli kufuatia malalamishi ya wakulima kuhusu uhaba wa maji.
Hata hivyo, walichana mbuga kuokoa maisha yao baada ya kundi la vijana wenye hamaki kufumania mkutano huo na kuwatimua.
Vijana hao waliwakashifu viongozi hao kwa kuibua sintohamu eneo hilo na kuchochea na vita.
Mtu mmoja alijeruhiwa wakati wa kioja hicho na alikimbizwa hospitalini ambapo alitibiwa na kuruhusiwa kuenda nyumbani.
Taifa Leo
Viongozi vijana wamekuwa wakimulikwa kwa kuonyesha mienendo mbaya kwa wanasiasa wengine chipukuzi nchini.
Wengi wao wamekuwa wakihusishwa katika skendo na kukiuka sheria.
Kukamatwa hii majuzi kwa Seneta wa Nairobi, Johnson Sakaja katika klabu moja kulizorotesha picha ya viongozi vijana.
Wengine ambao wamejipata pabaya na mkono wa sheria ni ikiwemo magavana Mike Sonko, Stephen Sang na wabunge Babu Owino, Charles Jaguar, Aisha Jumwa na waziri wa zamani Rashid Echesa.
READ ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdja4Z0gZZmpJqfka%2BytbWMsphmoqWirq%2B6xKOspZmZYn9yrtSnnp5lnJbEprfEsJhmpJ%2BYuKW71ppkpK2Wqq61tcBmpJqZlp7AonmUaWSkraCWwbitjKeYZpufq7aleZByZaGsnaE%3D