Maafisa wa polisi katika Kaunti ya Kilifi wanachunguza kisa ambapo watu wasiojulikana walifukua kaburi na kutoweka na mwili wa maiti.

Taarifa zinasema kuwa kaburi la marehemu Fatuma Maro liliachwa wazi kwani wezi hao pia waliondoka na jeneza kulingana na ripoti ya K24 Digital.

Habari Nyingine: Wafanyakazi wa Kaunti ya Kisii Waagizwa Kufanyia Kazi Nyumbani

Marehemu alizikwa miezi mitatu iliyopita huko Mazeras, eneo la Mabirikani katika Kaunti ya Kilifi.

Kulingana na mwanamwe mwendazake Stanley Lwambi, wanashuku kuwa tukio hilo limechochewa na mzozo wa ardhi baina ya familia ya bwenyenye fulani wa Kiarabu.

Alisema bwenyenye huyo ambaye hajulikani amekuwa akidai umiliki wa kipande cha ardhi ambapo mamake alizikwa.

Familia hiyo imeripoti kisa hicho kwa polisi ambao wameanzisha uchunguzi.

Habari Nyingine: Aden Duale Ataka Chama cha Jubilee Kilipe Deni la KSh 6 Milioni la Mwendazake Kalembe Ndile

Kamanda wa Polisi eneo la Rabai Fred Abuga, ambaye alizungumza na K24 Digital kwa simu, alithibitisha kisa hicho na kusema uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na tukio hilo la kutatanisha.

“Tulipata ripoti jana kwamba mwili umefukuliwa na haupo. Bado hatujapata habari zaidi kumhusu muhusika mkuu na nia yake haswa ilikuwa nini. Maafisa wetu wanachunguza kisa hicho,” alisema.

Kwingineko ni kuwa takriban wiki moja iliyopita mwili wa Elijah Obuong, mmoja wa wahasiriwa wanne wa Kitengela ulifukuliwa kaburini na kutoweka mnamo Jumatano, Juni 2 usiku.

Habari Nyingine: Eswaka, ugali mzito unaoliwa Baridi na Unaoweza Kuhifadhiwa Zaidi ya Wiki Bila Kuharibika

Kamanda wa Polisi kaunti ya Kisumu Samuel Anampiu alithibitisha kisa hicho akisema kuwa kundi la watu saba lilichimbua kaburi, wakachukua mwili wake na kuzika jeneza tupu.

Saba hao walifunika kaburi hilo kabla ya kuuweka mwili wake kwenye gari walilokuwa nalo na kuhepa ripoti ya The Standard ilisema.

Obuong alizikwa nyumbani kwa shangazi yake mnamo Mei 13, baada ya kudhulumiwa na kisha kuuawa katika kesi ambayo ingali inachunguzwa.

Anampiu alishuku kuwa mtu wa familia ambaye anasemekana hakufurahishwa wakati mhasiriwa alipozikwa kwa shangazi yake ndiye alihusika katika kuufukua mwili huo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZoF6hY9mrp6ymWLEorLUpKyaZZuWr7a%2ByGalmmWbqsGww8SkmGamkWK6uLXLomSupJmkx6q31ppkpqGVr7Zuf4yio6Kxn6W2ta2NoaumpA%3D%3D